Haile Gebrselassie astaafu riadha

Nguli wa mbio Haile Gebrselassie akifurahia ushindi.
Haile Gebrselassie ametamka bayana kustaafu mbio za ushindani .Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka arobaini na miwili mwenye asili ya nchi ya Ethiopia amethibitisha maamuzi yake ya kustaafu ukuzaji upepo,na hii ni mara baada ya kuhitimisha mbio za kumi na sita za Great Manchester mapema Jumapili.
Maamuzi haya yanahitimisha safari ya miaka ishirini na mitano ya ufukuzaji upepo safari ambayo iliwahi kumpatia medali mbili za dhahabu za michuano ya Olympic ,ushindi wa mara nane wa dunia wa riadha na kuweka rekodi duniani ya kufanya vyema mara ishirini na saba katika mbio kubwa duniani.
Mwenye Haile Gebrselassie anasema kwamba
‘nastaafu mbio za ushindani,sio kustaafu kukimbia!,huwezi kuacha kukimbia ,mbio ni maisha yangu, ameyasema haya nguli huyo wa ufukuzaji upepo alipokuwa akifanya mahojiano na shirika la BBC kitengo cha michezo.
Gebrselassie nabakia kuwa mkimbiaji mwenye rekodi ya kipekee tena mashuhuri katika mbio za mita elfu mbili duniani alizozimaliza kwa muda wa saa moja.
Suala la kutaka kustaafu riadha alilisema miaka mitano iliyopita na ni baada ya kupata ajali michezoni lakini akarejea katika mbio miezi kadhaa baadaye.
Gebrselassie alishindwa kuonesha uwezo wake adhim kabisa katika mbio za London za Olympic mwaka 2012 lakini si haba alishinda t mbio za the Great Scottish huko Glasgow nazungumzia mwaka mmoja baadayea, na tena akaendelea kusumbua katika mbio za Vienna City katika mbio za nusu marathon.
Sasa baada ya kung’ara katika mbio za ushindani za mwishoni mwa wiki mjini Manchester mbio ambazo amwekuwa kinara wa ushindi kwa miaka mitano mfululizo na kumaliza mbio ambazo amekuwa akizifurahia mara zote.
Ninayo furaha kusita hapa ama kuachia hapa nilikuwa najua fika kuwa hii ni mara yangu ya mwisho kuufukuza upepo amesema nguli huyo za mbio za Maratho anayetambulika fika katika ulimwengu wa michezo na dunia kwa ujumla.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart