Rais wa Chad, Idriss Deby, amesema kuwa vita dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram vinatatizwa na ushirikiano m'baya kati ya majeshi yake na yale ya Nigeria.
Akizungumza katika ziara rasmi nchini Nigeria, Bw Debby alisema kuwa kuna hatua zilizopigwa tangu Chad ijiingize katika vita dhidi ya wapiganaji hao.
Hata hivyo amesema ikiwa wanajeshi hao wangekuwa wakishirikiana wangekuwa wameliangamiza kundi hilo kwa sasa.
Chad na jirani yake Niger zilifanya mashambulizi dhidi ya kundi hilo la wapiganaji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwaka uliopita.