Kocha
 wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger 
baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango
 lake.
Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni 
rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema 
kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa 
katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.
