Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji FRANCIS MUTUNGI
Mkutano huo umehudhuriwa na vyama vya siasa ishirini na viwili nchini pamoja na asasi mbalimbali kujadili namna bora ya kushirki katika uchaguzi mkuu kwa amani bila kuharibu tunu ya taifa ambayo ni AMANI.
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji FRANCIS MUTUNGI amefungua mashauriano hayo na kusema wanasiasa wanapaswa kuimarisha demokrasia na kuwa na maridhiano badala ya kufanya kampeni za kukamiana ama kukomoana
Wakiwasilisha mada katika mkutano huu wadau wa siasa na maendeleo wamevishauri vyama vya siasa kutekeleza kazi zao kwa kuzingatia itikadi zao badala ya kuwa kama wanaharakati na pia kushirikisha makundi yote katika jamii yakiwemo vijana na wanawake kwakuwa idadi kubwa ya wananchi ni vijana lakini kwa upande wa jinsia wanawake ndio wengi.
Katika hatua nyingine msajili wa vyama vya siasa amevishauri vyama vya upinzani vinavyotaka kuungana kuwa na kauli moja ya nia hiyo na kupendekeza kubadilishwa kwa sheria kwakuwa kwa sasa sheria hairuhusu muungano wowote wa vyama vya siasa.