Tetemeko kubwa la ardhi limekumba eneo lililo magharibi mwa Nepal.
Shirika
la utafiti la Marekani liliseme kuwa tetemeko hilo la vipimo vya 7.9
lilikumba eneo lililo umbali wa kilomita nane mashariki mwa Pokhara
magharibi mwa mji mkuu wa Kathmandu.Kuna ripoti za uharibifu wa majengo. Idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa haijulikani.
Mawasiliano ya simu nayo yameharibiwa.
Walioshuhudia walisema kuwa watu walikimbia nje ya majengo muda mfupi baada ya tetemeko hilo kutokea.