Ikulu
ya white house nchini Marekani inasema kuwa rais Obama ana uhakika kuwa
Marekani itaafikia makubaliano ya mwisho na Iran kuhusu mpango wake wa
nyuklia ifikiapo mwishoni mwa mwezi Juni.
Msemaji wa Ikulu anasema
kuwa bado kuna kazi ya kufanywa kwa yale yaliyoafikiwa siku ya alhamisi
licha ya wanasayansi waliyoyachunguza maafikiano hayo kusema kuwa wana
uhakika kuwa yanaweza kuizuia Iran kuunda silaha za nyuklia.Msemaji huyo wa ikulu ameongeza kuwa Marekani haitatia sahihi makubaliano ambayo yataiweka Israeli hatarini akisema kuwa Marekani inaendelea kushauriana na washirika wake katika eneo hilo.
Rais wa Iran Hassan Rouhani anasema kuwa nchi yake itaheshimu upande wake wa makubaliano hayo iwapo wengine nao watafanya hivyo.