Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira, Dr BINILITH MAHENGE
Waziri MAHENGE amezindua miradi hiyo sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa kufundishia somo la Mazingira kwa wanafunzi wa shule za Msingi.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa kuiwezesha jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, na Mradi wa upandaji wa miti ili kuboresha hifadhi ya misitu iliyoharibiwa na watu wasiojulikana kuzunguka wilaya za Iringa Vijijini na Makete, mkoani Njombe.
Aidha idadi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mengi yamekuwa yakipata msaada wa fedha za wahisani ili kuwasaidia wananchi kujua mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira, lakini baadhi ya viongozi wa mashirika hayo wamekuwa wakijinufaisha wao wenyewe.