Diamond akabidhiwa milioni 14 za ujenzi

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya.
Pesa hizo ni kwa ajili ya ukarabati wa ukuta wa nyumba yake ambao uulidondoka kutokana na mvua
Pesa hizo ni kwa ajili ya ukarabati wa ukuta wa nyumba yake ambao uulidondoka kutokana na mvua
“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond huku akiwataka Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga, aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni ya gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart