Australia yaomba Japan kutowaua raia wake

raia wa Australia wanaotarajiwa kunyongwa kwa kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya mihadarati
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbot amesema amemuandikia barua rais wa Indonesia Joko Widodo akimuomba awasamehe raia wawili wa Australia ambao walipatikana na hatia ya kuendesha biashara ya madawa ya kulevya. Awali rais Widodo alikataa kuzungumza na bwana Abbot kwa njia ya simu.
Waustralia hao wawili wamejulishwa kuwa watauawa ifikiapo kesho Jumanne.
Wawili hao walihukumiwa mwaka 2006 kwa kuongoza kundi moja lililojaribu kusafirisha dawa ya heroin kutoka nchini Indonesia.
Wawili hao ni baadhi ya raia wa kigeni waliohukumiwa kifo na ambao wamejulishwa kuwa hukumu zao zitatekelezwa siku chache zinazokuja.
Naye rais wa Ufilipino (Benigno Aquino) amemuomba rais Widodo kumpa msamaha mwanamke raia wa nchi hiyo (Mary Jane Veloso) ambaye ni mmoja wa wale wanaosubiri kuuawa.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart