Rais
Obama amemtumia salaam za pongezi waziri mkuu wa Israel, Benjamin
Netanyahu kutokana na ushindi uliokipata chama chake katika uchaguzi
uliofanyika Jumanne.
Lakini Bwana Obama ameelezea dhamira yake ya
kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na Wapalestina kuwa ni kuunda
taifa la Palestina.Awali Ikulu ya Marekani ilielezea wasiwasi kuhusu ahadi ya Bwana Netanyahu wakati wa kampeni za uchaguzi kwamba asingeruhusu kuundwa kwa taifa la Palestina.
Waziri mkuu wa Israel tangu wakati huo amelegeza msimamo wake, akisema atakubali suluhisho la kuwepo mataifa mawili jirani endapo usalama katika eneo la Mashariki ya Kati utaimarishwa.