Mwanamke wa pili kuwa askofu kwenye kanisa la Anglikana


Askofu Canon akiwa na wachungaji wenzake
Askofu Canon akiwa na wachungaji wenzake
Kanisa la anglikana nchini Uingereza limemteua Askofu wake wa pili mwanamke Canon Alison White ambaye pia mumewe Frank, naye ni Askofu wa kanisa hilo.
Canon White atakuwa naibu Askofu katika Jimbo la Hull, na mumewe ni Naibu askofu wa jimbo la Newcastle.
Alison alikuwa msimamizi wa parokia katika Riding Mill katika Jimbo la Northumpland.
Watu hao wameweka historia ya mume na mke kuwa maaskofu katika kanisa hilo.
Mama huyo alitawazwa kuwa deacon mwaka 1987 na akawa kasisi wa kanisa mwaka 1994.
Askofu mtarajiwa huyo amesema  kuwa kwa wao kuwa maaskofu kwenye familia ni changamoto kubwa lakini akahakikishia waumini wanaendelea na kazi yao kikamilifu kutokana na ujuzi wa ndoa walionao wa zaidi ya miaka 30.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart