Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.
Aidha Marekani pia imetoa tahadhari kwa raia wake.Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.
Katika kipindi kilichopita, kundi la Al-Shaabab lenye makao yake Nchini Somalia, limetekeleza mashambulio Nchini Uganda.