Marekani yachapwa 3 -2 na Denmark

Mechi kirafiki za kimataifa zilizopigwa usiku wa kuamkia leo ambao Scotland iliwashikisha adabu ndugu za Ireland ya kaskazini baada ya kuwanyuka goli moja kwa bila majibu.
Goli hilo la dakika za lala salama lilifungwa Christopher Berra dakika ya 85 kwa njia ya kichwa baada ya kona iliyochongwa na Matt Ritchie.
Katika mechi nyingine Geogia iliwaadhibu Malta kwa jumla ya mabao 2 - 0 , huku Denmark
Timu ya taifa ya Marekani
ikiwageuza nyanya Marekani baada ya kuwatundika mabao 3 kwa 2.
Kwa upande Ujerumani ilishikwa sharubu na Australia baada ya kutoka sare ya magoli mawili kwa mawili.
Leo kutakuwa na mechi nyingine za kirafiki ambapo Ufaransa wakuwa wenyeji wa Brazil huku Bahrain wakikutana uso kwa uso na Colombia.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya Iran ambao wataumana vikali na Chile.

Post a Comment

http://www.princetarique.blogspot.com

Previous Post Next Post

Comments System

blogger/disqus/facebook

Disqus Shortname

designcart