Mkuu wa wilaya ya KINONDONI, PAUL MAKONDA
MAOFISA wa ardhi nchini wametakiwa kuwa waaminifu katika kazi zao
ili kuepuka migogoro ya ardhi inayotokea kila kukicha katika maeneo
tofauti ya nchi.
Mkuu wa wilaya ya KINONDONI, PAUL MAKONDA ameyasema hayo wakati alipokutana na umoja wa mafundi wa magari katika eneo la TEGETA ambao wana mgogoro wa ardhi na mwekezaji NYAZA ROAD WORKS.
MAKONDA amesema Maofisa ardhi ambao si waaminifu wamekuwa wakiuza maeneo ya ardhi ambayo tayari wameshauziwa watu wengine kwa kutumia ramani tofauti
Aidha , MAKONDA amesema katika manispaa ya KINONDONI pekee rekodi zinaonyesha kwamba kila mwezi wanapokea kesi zinazohusu ardhi katika manispaa hiyo takribani kesi 1,600 kutoka kwa watu binafsi au taasisi, hivyo ni wakati wa kulifanyia kazi suala hilo.