Kocha
 wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema ingeshangaza sana kama 
mchezaji kinda wa klabu ya Tottenham Harry Kane asingejumuishwa katika 
kikosi cha Nchi hiyo kinachotarajiwa kumenyana na Lithuaniana na Italy.
Mchezaji
 huyo mwenye umri wa miaka 21, ni miongoni mwa wachezaji 24 wa kikosi 
cha England ambacho kimetajwa na Hodgson kucheza dhidi ya Lithuania 
mchezo ambao utapigwa katika dimba la Wembley mnamo march ,27 mwaka huu 
 kwaajili ya mechi za kufuzu katika mashindano katika  mataifa ya Ulaya 
yanayotarajia kufanyika mwakani. Kikosi hicho pia kinatarajia kuumana na
 Italy katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa mjini Turin huko Italy 
tarehe 31 mwezi huu.