Mwasisi wa shirika la Microsoft linalojihusisha na programu za kompyuta
Bill Gates ametoa wito wa kutengenezwa michezo ya kompyuta inayotoa
mafunzo badala ya ile ya vita.
Bill Gates amesema ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kama Ebola ni bora kutengeneza michezo ya kompyuta inayotoa mafunzo kama michezo kuhusu vijidudu maradhi badala ya ile inayohusu vita na mapigano.

Bill Gates alisema hayo wakati alipokuwa anakabidhi vifaa vya
kukabiliana na ugonjwa wa ebola ya kutibu na ameongeza kuwa utengenezaji
wa michezo ya kompyuta inayotoa mafunzo inaweza kutoa uwezo wa
kuzidisha maarifa ya watu kuhusu magonja mbalimbali na njia za
kukabiliana nayo.
Wataalamu wengi wa elimu binafsi wamekuwa wakikosoa michezo ya kompyuta
inayotengenezwa katika nchi za Magharibi ambayo nyingi inahusiana na
utumiaji mabavu, ukatili, vita na hata utovu wa maadili