1. Badilisha mavazi yako .
Ikiwa
bidhaa za kampuni unayoipenda zinabadilika baada ya miaka michache ili
kupata umaruufu kwa wateja wake,pia wewe badilisha sura yako kwa
kubadilisha mavazi na mfumo wa nywele ili umfurahishe mpenzi wako.....>>>>Hata kama umekuwa ukipendeza kwa mavazi yako, mpenzi wako tayari amekuzoea hivyo.
Nunua nguo mpya, chupi mpya, jaribu mtindo mwingine wa kutengeneza nywele ndiposa mpenzi wako akuone kama mgeni vile.
2. Hamia nyumba mpya
Ukiwa umekuwa ukiishi katika mtaa mmoja kwa miaka mingi ,badilisha maeneo yako.
Gura kwenda kwenye mtaa mpya, hili litakusaidia Kubadilisha mazingira na itaisisismua akili na kufurahia mukiwa pamoja.
3. Badilisha mfumo wa chumba chako cha kulala.
Panga vitu upya,ondoa vitu za kitambo,nunua vitu vipya,paka rangi tofauti tofauti kwenye ukuta wako.
Chumba cha kulalia kinapaswa kuwa cha kuvutia mno, badilisha mipangilio ya chumba chako mukiwa pamoja na mpenzi wako ndivyo nyiyi wote mumiliki mabadiliko hayo.
4. Omba msamaha nawe umsamehe.
Ni vigumu kuwa na urafiki wakati masuala tata kati yenu hayajatatuliwa.
Usipuuze maswala ambayo ni kawaida katika uhusianio,upendo wa dhati sio eti kwa sababu hamgombani wewe na mpenzi wako
Upendo wa dhati ni uwezo wa kusuluhisha matatizo kati yenu.
Omba msamaha wakati umekosea nawe msamehe wakati umekosewa.
5. Endeni mjivinjari kwa tarehe
Endeni likizo au tokeni nje pamoja.
Mkiwa nyote kwenye kwenye mazingira mapya inaweleta nyote pamoja.
6.Kataeni hamu ya kutizama picha za kujamiana.
Watu wengi wanaohusiano hudhani kuwa kuangalia picha hizo za kujamiana ni kitu kizuri ilhali ni jambo hatari sana.
Jiulize mbona watu huangalia picha hizi?
Kwa ajili ya kusisimua hali yao ya ngono?.
Kutegemea picha hizi kusisimua fataki kati yenu inamyang'anya mpenzi wako mamlaka ya kukusisimua mwenyewe.
Je inammanisha kuwa mpenzi wako hawezi kukusisimua?
Kama ni hivyo picha hizi hazisaidi kutengeneza hali zinaharibu.
Picha hizi zinafanya mapenzi yawe duni ilhali ni mmoja wapo wa kuwa na mapenzi.
Rudisha mapenzi na uwacha picha hizo mbaya ndiposa mpenzi wako aweze kujisalamisha kwako na ni jukumu lenu kusisimuana hisia kali za mahaba ile umruhusu awe spesheli kwako nawe kwake.
7. Jisalimishe upya
Kama fataki katika yenu yamekuwa yakididimia tatizo ni lenu.
Je unampenda kama awali?
Je unanipenda kweli?
Ondoa hofu hizo kwa kumhakikishia penzi lenu.
Hii ndiyo sababu wapenzi husherekea penzi lao.
8. Weka mtoto mbali na maswala yenu ya Huba.
Ni vizuri kuwa na watoto na kuwa karibu nao lakini wakti mwengine ni vyema watoto kuwa mbali na wazazi ili waweze kuwa na mda wao wa kipekee .
Tunza watoto kutokana na penzi lenu, penzi lenu likiingiiliwa kati basi uwezo wenu kama wazazi utaadhirika.
9. Epuka kuumiza mwenzako
Punguza visa vya kumuudhi na kumumiza mwenzako.
Roho iliyoumizwa ni vigumu kupenda.
10. Mbusu mpenzi wako zaidi.
Mabusu huleta watu pamoja.
Unavyo mbusu zaidi ndivyo munavyo chochea penzi.
11. Omba
Mungu anajali kuhusu penzi lenu na ndoa yenu.
Ombeni kwa pamoja kuhusu shida za penzi lenu.
12. Tenga wakati wa Faragha
Tenga wakati mahsusi kwa mpenzi wako.
Wanandoa wengi huwa na wakati mgumu sana kutenga muda maalum kuwa na wapenzi wao kutokana na majukumu ya maisha kama vile kazi safari watoto na kadhalika lakini
Jitahidi uweke kando muda maalum ambao utakaa karibu naye msemezane
Mkumbatiane mkumbushane haswa mlikotoka na mnakokwenda .
Ni muhimu sana.
13. Usilete majukumu yako ya kikazi nyumbani.
Ni vyema kufanya kazi ili kujipatia riziki yako na familia yako lakini kazi hiyo isalie kule afisini wala isiletwe nyumbani kamwe.
Usije na kazi yako ndani ya chumba chenyu cha kulala au ufanye mpenzi wako ahisi kuwa unamnyanyasa kwa sababu licha ya kuwa ulimuuowa mpenzi wako lakini umeoleka kwa kazi yako.
14. Weka teknolijia mbali
Teknolojia ni nzuri maanake inakupasha yanayojiri papo hapo .
Pia inawakutanisha hata mkiwa mbalimbali ,lakini ukiwa na mpenzi wako mbona usiiweke hiyo simu ama Kompyuta mbali ?
Mpenzi wako anataka kuongea nawe,kukubusu,kukumbatia kuwa karibu yako anataka kuisikia sauti yako lakini macho yako yanijishughulisha na kuongea kwa simu,mtandao wa kijamii ama unachapisha ujumbe .
Je nayeye akianza kuienzi kompyuta yake kuwasabahi jamaa na marafiki kwenye mitandao ya kijamii kutakuwepo na ndoa ?
Ukiwa nyumbani na mpenzi wako jiepushe na Teknolojia .
15. Chezeni pamoja
Kucheza pamoja kunaimarisha mahaba.
Haijalishi kama mpenzi wako anajua kupiga densi zaidi yako au la , Mkiwa pamoja weka mziki anaoupenda kisha mwite aje mpige naye rhumba,salsa Bongo flava, reggae ,hip hop hata Chakacha kama ni mwenyeji wa pwani !
Chezeni miili yenu ikigusana!
16 Kaeni msemezane
Mkiwa kitandani na mpenzi wako mnazungumza ?
Unamwambia nini kitandani ?
Unazungumzia kuhusu madeni yako?
Usidhubutu ,mwambie kuhusu mahitaji yenu ya kimahaba ,mwambie unampenda na kuwa haujui ungelikuwa wapi bila yeye .
17. Andikianeni barua za kimapenzi.
Mwandikie barua za kimapenzi na uiache kwenye gazeti au kwenye tarakilishi ,kitu ambayo itamfanya afurahie,kutoka kwa mwandiko wako.
18. Puuza watu ambao watakuvuruga amani kati yenu
Hao watu wanaokutongoza kupitia kwenye mitandao ya kijamii ima ni Facebook,WhatsApp wazuie wasikutumie ujumbe wa moja kwa moja.
Ni mahasidi hao,wala hawakupendi Ng'ooooo!!!!
Wao wangalikupenda kweli hawangejaribu kukuletea huzuni kwa kuvunja penzi/ndoa yenu.
Kujihusisha nao inapunguza makali ya penzi lenu ukidanganyika kuwa unapendwa ilhali ni Wanafiki tu
19.Nunua marashi mapya
Mnunulia mpenzi wako marashi yanayonukia vyema yatakayo fanya mpenzi wako afurahie kuwa nawe.
20.Jiachilie
Kuwa na uwazi wa mawazo ukiwa na mpenzio
Jaribu njia tofauti za kufanya mapenzi
Zungumzeni kama ambao mnaigiza sinema za mahaba
Mchezee shere
Mtanie mpenzi wako