Wana
wawili wa aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wameachiliwa kutoka
jela, miaka minne baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa pamoja na baba
yao.>>>>>
Wakuu wa gereza wanasema kuwa Gamal na Alaa Mubarak wote wanabiashara maarufu waliachiliwa mapema leo Jumatatu.Juma lililopita mahakama iliamuru kuachiliwa kwao huku kesi dhidi yao kuhusu ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, ikiendelea.
Mubarak anaendelea kuzuiliwa katika Hospitali moja ya kijeshi, ambapo anatumikia hukumu ya matumizi mabaya ya pesa za umma.