Raia wa japan kuwachagua wabunge wapya
Raia wa Japan wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa ubunge
ulioitishwa mwezi uliopita na waziri mkuu Shinzo Abe wakati ambapo
anatafuta uungwaji mkono katika mipango yake ya mabadiliko ya kiuchumi.
Abe pamoja na chama chake cha Liberal Democratic wanatarajiwa kushinda licha ya Japan kurejea tena kwenye hali mbaya ya uchumi.Bwana Abe alichukua mamlaka mwaka 2012 ambapo aliahidi kuikwamua Japan kutoka kwa miongo miwili ya misukosuko ya kiuchumi.