Jenerali Sejusa aliyeitoroka uagnda baada ya kutofautiana na rais Musevenei hadharani
Jenerali Sejusa aliyeitoroka uagnda baada ya kutofautiana na rais Musevenei hadharani
Mwanajeshi
wa Uganda a
mbaye alitofautiana hadharani na rais wa nchi hiyo Yoweri
Museveni mwaka uliopita amerejea nchini Uganda bila kutarajiwa kutoka
nchini Uingereza ambapo alikuwa amekimbilia uhamishoni.
Jenerali
David Sejusa aliitoroka Uganda baada ya kumshutumu rais Museveni kwa
kujaribu kubuni familia ya kifalme akitaka kumkabidhi uongozi mwanawe wa
kiume.
Sejusa pia alidai kuwa kulikuwa na njama ya kuwaua watu fulani katika serikali na jeshini ambao walikuwa wakipinga mpango huo.
Rais Museveni anayedaiwa kumtayarisha mwanawe ili kuchukua utawala wa Uganda
Alipowasili mjini kampala
Jenerali Sejuse alikutana na mkuu wa ujajusi ambapo pia aliwaambia
waandishi wa habari kuwa rais Museveni alifahamu kuhusu kurejea kwake.